89462916_892424224547433_9039089720871758910_n

NA NICKSON TOSI

Mtangazaji wa televesheni ya humu nchini Betty Kyallo amezungumza kwa mara ya kwanza na kuwashukuru wote wanaomshabikia katika kazi yake, siku chache tu baada ya video yake kuibua gumzo mitandaoni.

Katika video hiyo, Betty aliwakashifu wanablogu wanaoingilia maisha yake ya kibinafsi bila hata ya kutafakari kuhusiana na athari za baadaye.

Miongoni mwa wale waliowakashifu wanaoingilia mwanahabari huyo ni mtangazaji Shaffie Weru ambaye alisema hivi.

Watu wanaomkashifu Betty ni lazima wastaarabike kwanza, hakuna mwanadamu mkamilifu maishani na sisi sote tuna ulegevu katika maisha yetu. Anza kujiangalia kwanza kabla ya kumkashifu mwenzio. Aliandika Shaffie

Mtetezi wa haki za kibinadamu Boniface Mwangi pia yeye alikuwa na haya ya kusema.
Betty hana deni la mtu na hastahili kuomba msamaha baada ya kujivinjari na kusherehekea maisha yake kutokana na jasho lake. Wacheni kuingilia maisha ya kibinafsi ya mtu ambaye hana deni lenu. Tumieni wakati wenu mlionao kuishauri serikali na viongozi mliowachakuwa kutekeleza miradi yao. Aliandika Mwangi.
 Hii hapa video ya Betty.