Asanteni mashabiki wangu! Betty awashukuru mashabiki wake baada ya Video yake kuenea
NA NICKSON TOSI
Mtangazaji wa televesheni ya humu nchini Betty Kyallo amezungumza kwa mara ya kwanza na kuwashukuru wote wanaomshabikia katika kazi yake, siku chache tu baada ya video yake kuibua gumzo mitandaoni.
Katika video hiyo, Betty aliwakashifu wanablogu wanaoingilia maisha yake ya kibinafsi bila hata ya kutafakari kuhusiana na athari za baadaye.
Miongoni mwa wale waliowakashifu wanaoingilia mwanahabari huyo ni mtangazaji Shaffie Weru ambaye alisema hivi.
Watu wanaomkashifu Betty ni lazima wastaarabike kwanza, hakuna mwanadamu mkamilifu maishani na sisi sote tuna ulegevu katika maisha yetu. Anza kujiangalia kwanza kabla ya kumkashifu mwenzio. Aliandika Shaffie
Hii hapa video ya Betty.
Betty baada ya video hiyo aliwashukuru wote wanaofanikisha ukuwaji wake kimaisha.