Triple Trouble : Wasichana watatu wa shule kutoka familia moja wapachikwa mimba
Familia moja huko Mbeere kusini katika kaunti ya Embu imeshindwa la kufanya baada ya wanao watatu waliokuwa wakisoma kupachikwa mimba muda huu ambao wamekuwa nyumbani baada ya shule kufungwa kwa ajili ya janga la corona
Wasichana hao wa darasa la saba, nane na kidato cha tatu wote walipimwa na kupatikana na mimba wakati kila mmoja wote alipoanza kuonyesha dalili za ujauzito. Baba yao Fred Njuki amesema baada ya ugunduzi kwamba binti zake wana mimba ameshinda atachukua hataua gani kwa sababu itakuwa vigumu kwake kuwatunza wakiwa na wanao. Kesi hiyo tayari ipo polisi na wasichana hao wanazidi kuhojiwa kuwataja watu waliowapachika mimba.
Njuki amesema wameanza kutafuta misaada kutoka kwa mashirika yasio ya kiserikali ili kuhakikisha kwamba binti zake wanarejea shuleni pindi tu watakapojifungua .
Wiki jana serikali imetoa takwimu zinazoonyesha kwamba wasichana 4000 walipachikwa mimba wakati shule zilipofungwa kwa ajili ya janga la corona. wizara za elimu na afya zimeanza kuchukua hatua ili kuzuia visa hivyo huku wasichana wengi wakiripotiwa kupachikwa mimba na wenzao.