Statehouse

  Rais Uhuru Kenyatta  amehamia jumba la Harambee baada ya ikulu kufungwa wafanyikazi wanne walipopatikana na virusi vya corona .

Rais Kenyata  amesema hajapatikana na virusi hivyo na amekuwa akifanya kaz katika jumba la Harambee  iliyotajwa kuwa salama .wafanyikazi wake pia wamehamia jengo hilo naye .

Rais Kenyatta amekuwa akifanyia kazi Ikulu ya Nairobi hadi  visa vya corona vilivporipotiwa Juni tarehe 15 katika makao hayo yake .mikutano yake yote sasa  imekuwa ikifanyika Harambee .

Kabla ya visa hivyo vya corona kuripotiwa Ikulu rais alikuwa akiandaa mikutano  yake  yote  ikiwemo na wabunge  na baadhi ya wanasiasa katika Ikulu .

View Comments