Baba Lao: Diamond Platinumz atikisa maungo na Hamisa na Wema katika usiku mmoja
Siku ya jumamosi msanii Diamond Platinumz aliandaa bash kubwa kwa hisani ya msanii wake wa kike Zuchu katia usiku uliowaleta pamoja wasanii wote tajika nchini Tanzania katika paa moja .
https://www.instagram.com/p/CC0ASHAA651/
Miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Lady Jay Dee, Mbosso, Juma Jux, maneja wa Diamond Sallam, Esma, Sandra Kassim, Rayvanny, Irene Uwoya, Jokate Mwegelo, wapenzi wa Diamond Wema Sepetu, Hamisa Mobetto miongoni mwa wengine wengi
Lakini kilichowapata wengi kighafla ni wakati Diamond alipoingia steji kupiga densi na Hamisa Mobetto na baadaye akizungumza baada ya hafla hiyo alimlimbikzia Hamisa sifa nyingi sana ;
NASHUKURU MOBETTO STYLES NDIO WAMENIVALISHA.NI DESIGNER NA MIMI KAMA MTANZANIA NINA KILA HAKI YA KUSUPPORT WATANZINIA WENZANGU.
Wakati mmoja pia Diamond alipata fursa kwenye steji kuzinengua na mpenzi wake wa zamani Wema walipokuwa wakiucheza wimbo a Mbossi ,Hodari .
https://www.instagram.com/p/CCzUP98gF1Y/
Video hizo mbili sasa zinasambazwa mitandaoni na wengi wanangoja kwa hamu kuona wapenzi wengine wa zamani wa Diamond Zari Hassan na Tanasha Donna watasema nini kuhusu video hizo