Lionel Messi  ameshinda tuzo yake ya saba ya mfungaji wa mabao mengi katika La liga  na yake ya nne mfululizo baada ya kuifungia Barcelonamabao mawili katika ushindi wao wa  5-0 dhidi ya kilabu ya  Alaves  katika siku ya mwisho ya ligi hiyo ya uhispania .

Nahodha huyo wa Barcelona alimaliza kwa mabao 25  ,manne mbele ya mshambuliaji wa Real Madrid Karim Banzema . mchuano huo hata hivyo haukuwa muhimu wa Barca kwani tayari walikuwa wameshalinyakua taji hilo siku ya alhamisi .

Messi  alifaulu kumkanganya mlinda lango ili  kufunga mabao mawili huku  Ansu Fati, Luis Suarez na  Nelson Semedo  wakifunga mabao mengine .

Riqui Puig, Messi  na Arturo Vidal wote waligonga mkuti kabla ya Fati kufungua mwanzo wa mabao .

Hii ndio ya kwanza  kwamfungaji bora wa La liga kufunga chini ya mabao 30  tangu  nyakati za Daniel Guiza wa Mallorca miaka 12 iliyopita .

View Comments