Lionel Messi ameshinda tuzo yake ya saba ya mfungaji wa mabao mengi katika La liga na yake ya nne mfululizo baada ya kuifungia Barcelonamabao mawili katika ushindi wao wa 5-0 dhidi ya kilabu ya Alaves katika siku ya mwisho ya ligi hiyo ya uhispania .
Nahodha huyo wa Barcelona alimaliza kwa mabao 25 ,manne mbele ya mshambuliaji wa Real Madrid Karim Banzema . mchuano huo hata hivyo haukuwa muhimu wa Barca kwani tayari walikuwa wameshalinyakua taji hilo siku ya alhamisi .
Messi alifaulu kumkanganya mlinda lango ili kufunga mabao mawili huku Ansu Fati, Luis Suarez na Nelson Semedo wakifunga mabao mengine .
Riqui Puig, Messi na Arturo Vidal wote waligonga mkuti kabla ya Fati kufungua mwanzo wa mabao .
Hii ndio ya kwanza kwamfungaji bora wa La liga kufunga chini ya mabao 30 tangu nyakati za Daniel Guiza wa Mallorca miaka 12 iliyopita .