Meja Jenerali Fatuma Ahmed ateuliwa mwanamke wa kwanza kuongoza jeshi la angani Kenya

Uteuzi wake umetangazwa na idara ya ulinzi baada ya kuidhinishwa na Rais William Ruto.

Muhtasari

•Meja Jenerali Fatuma Ahmed ameandikisha historia nchini Kenya kwa kuteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza kitengo cha jeshi la angani.

•Jenerali Ahmed alianza kazi ya uanajeshi mnamo 1984 alipojiunga na Jeshi la Kenya.

Image: BBC

Meja Jenerali Fatuma Ahmed ameandikisha historia nchini Kenya kwa kuteuliwa kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza kitengo cha jeshi la angani katika majeshi ya Ulinzi wa Kenya, KDF.

Uteuzi wake umetangazwa na idara ya ulinzi baada ya kuidhinishwa na Rais William Ruto ambaye pia amemteua Jenerali Charles Kahariri kuwa mkuu wa majeshi.

Jenerali Kahariri alikuwa anashikilia wadhifa huo akiwa Luteni Jenerali baada ya kifo cha Jenerali Francis Omondi Ogolla mwezi Aprili katika ajali ya ndege.

Meja jenerali Ahmed amekuwa mwanamke wa kwanza katika miaka kumi iliyopita kupandishwa cheona kuwa Brigedia na tena kuwa Meja Jenerali na kuongoza taasisi muhimu katiika jeshi kama vile kuwa kamanda wa chuo cha mafunzo ya kijeshi cha KMA kule Lanet katika kaunti ya Nakuru.

Kabla ya uteuzi wake alikuwa katika chuo kingine cha mafunzo cha National Defence College mjini Nairobi kama mmoja wa wakurugenzi.

Jenerali Ahmed alianza kazi ya uanajeshi mnamo 1984 alipojiunga na Jeshi la Kenya.

Mwaka mmoja baadaye, alijiunga na chuocha mafunzocha KMA na kupata mafunzo ya kijeshi na kitaaluma kabla ya kufuzu na kuwa Luteni kiwango cha chini na kuwa katika kitengo maalum cha kina dada katika jeshi cha Womens corps.

Baada ya kuvunjwa kwa kikosi hicho alijiunga na jeshi la angani Kenya Airforce na kujukumikia kazi zake katika taasisi mbali mbali kwenye kambi za jeshi la angani za Moi Air Base Nairobi na Laikipia Airbase Nanyuki.

Mnamo 2017 Rais Uhuru Kenyatta alimteua kuwa Brigedia wa kwamza wa kike katik jeshi la Kenya na baada ya uteuzi wake mabadiliko makubwa ya kuwajumuisha kina mama katika uongozi jeshini yameshuhudiwa kama katika kitengo cha mawasiliano ambacho kinaongozwa na Brigedia Ziporra Kioko, kitengo cha sheria kinachoongozwa na Brigedia Yvonne Kerubo na mkurugenzi wa tasisi ya usalama na amani IPSTC Brigedia Joyce Sitienei , na afisa anayesimamia kitengo cha kubuni ramani Brigedia Caroline Mutisya .

Katika uteuzi wa alhamisi hii Rais ammeteua meja jenerali John Omenda ambaye alikuwa mkuu wa jeshi la angani kuwa Luteni Jenerali na kushikilia wadhifa wa naibu mkuu wa majeshi, Meja jenerali Paul Owuor amekabidhiwa wadhifa wa mkuu wa jeshi la majini huku maafisa wengine wakipandhiswa madaraka kutoka Ubregedia na kuwa meja jenerali na kuteuliwa pia kuongoza tasisi mbali mbali