Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka  ametnagaza mipango ya kujiondoa rasmi kutoka muungano wa NASA unaoongozwa na Raila Odinga ili kujiunga na   Jubilee .

Kamati ya usimamizi wa chama cha Wiper  ilikutana kupitia njia ya mtandao na kupitisha uamuzi wa  kujiunga katika muungano na chama cha Jubilee kinachoongzowa na rais Uhuru Kenyatta .

Hatua hiyo sasa inamaanisha kwamba  iper sasa itaondoka kutoka muungano huo wa upinzani kwani sheria  hairuhusu chama kimoja kuwa katika zaidi ya muungan mmoja .

Chama cha Kalonzo pia kitalazimika kumuandikia msajili wa vyama Anne Nderitu kumfahamisha rasmi kuhusu uamuzi wa kujiondoa kutoka NASA na kuiunga na muungano mpya .

Ili muungano wa NASA kuvunjiliwa mbali kabisa vyama tanzu  vitatu vinafaa kuondoka  lakini kwa sasa ODM ,ANC na Ford Kenya bado vipo katika muungano huo .

View Comments