Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ametnagaza mipango ya kujiondoa rasmi kutoka muungano wa NASA unaoongozwa na Raila Odinga ili kujiunga na Jubilee .
Kamati ya usimamizi wa chama cha Wiper ilikutana kupitia njia ya mtandao na kupitisha uamuzi wa kujiunga katika muungano na chama cha Jubilee kinachoongzowa na rais Uhuru Kenyatta .
Hatua hiyo sasa inamaanisha kwamba iper sasa itaondoka kutoka muungano huo wa upinzani kwani sheria hairuhusu chama kimoja kuwa katika zaidi ya muungan mmoja .
Chama cha Kalonzo pia kitalazimika kumuandikia msajili wa vyama Anne Nderitu kumfahamisha rasmi kuhusu uamuzi wa kujiondoa kutoka NASA na kuiunga na muungano mpya .
Ili muungano wa NASA kuvunjiliwa mbali kabisa vyama tanzu vitatu vinafaa kuondoka lakini kwa sasa ODM ,ANC na Ford Kenya bado vipo katika muungano huo .