Raila awataka maseneta kuunga mkono mfumo wa CRA wa ugavi wa mapato
Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewataka maseneta kupitisha mfumo wa ugavi wa mapato ulipendekezwa na tume ya CRA
Kupitia taarifa Raila amesema senate inafaa kuruhusu taifa kundelea mbele baada ya kushindwa kupata mwafaka kuhusu mbinu inayofaa kutumiwa kugawa pesa hizo kwa kaunti . marekebisho ya mfumo huo yalikuwa yamependekezwa na senate.
" Chini ya hali hii nchi yetu na wananchi sasa watahudumiwa vyema endapo tutatumia mfumo uliokuwa umependekezwa na tume ya CRA’ amesema Raila
Raila amesema masuala mengine yanayoibuliwa yanaweza kupelekwa kwa CRA Ili kuzingatiwa katika siku zijazo .
Taarifa ya Odinga imejiri baada ya kuzuka mgawnayiko kati ya maseneta kuhusu jinsi pesa za kauti zinazofaa kugawanya baada ya kuzuka tofauti kuhusu mbinu mbili za kutumika katika kuamua kiasi ambacho kila kaunti itapokea .
Kiraranja wa wengi katka senate Irungu kangata hata amenukuliwa akisema kwamba akisema mwafaka wa handshake utakuwa hatarini endapo mfumo unaopendekezwa na serikali hautapitishwa .