logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Sonko kugharamia mazishi ya Kevin Oliech

Sonko kugharamia mazishi ya Kevin Oliech

image
na

Burudani01 October 2020 - 09:44
Gavana wa Nairobi Mike Sonko  attoa sehemu ya gharama ya mazishi ya  Kevin Oliech ambaye aliaga dunia mwezi ulioppita .

Kevin  ni kakake mchezaji wa zamani wa Harambee Stars Denis Oliech na aliaga dunia kutokana na kansa  katika hospitali moja mjini Berlin ,Ujerumani agosti tarehe 16 mwaka huu .

Kupitia twitter , Sonko amesema atalipia baadhi ya gharama za mazishi ya Kevin . amesema alimjua marehemu kupitia kakake Denis  huku akimsifia kama mwanasoka stadi ka tu kaake Denis .

Kevin alizichezea timu za Nairobi City Stars kisha baadaye Mathare United .Mwili wake utawasili katika uwanja wa ndege wa JKIA  siku ya alhamisi .

Utahifadhiwa katika  Umash Funeral Home  kisha usafirishewe siku ya ijumaa  kwa mazishi Seme siku ya jumamosi .

 

Maarufu Zaidi

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2026. All rights reserved