24 September 2020 1 Min Read
Wabunge waidhinisha uteuzi wa Anne Nderitu kama msajili wa vyama vya kisiasa
by Yusuf Juma Habari
Kamati moja ya bunge siku ya alhamisi imeidhinisha uteuzi wa Anne Nderitu kama msajili wa vyama vya kisiasa .
Nderitu amekuwa akishikilia nafasi hiyo kwa muda tangu mwaka wa 2018 alipochukua usukani kutoka kwa Luvy Ndung’u aliyehamia tume ya Haki
Jamati ya haki na masuala ya sheriapia imewaidhinisha Ali Abdullahi na Florence Tabu kama manaibu wa msajili wa vyama
Kamati hiyo inayoongozwa na Kigano Muturi hata hivyo imekataa kumwidhinisha Wilson Mohochi kama naibu wa msajili
Rais Uhuru Kenyatta alimteua Nderitu kuchukua kazi hiyo Septemba tarehe 8 .Kabla ya kuichukua akzi hiyo Nderitu alikuwa mkuu wa usajili wa wapiga kura katika tume ya uchaguzi.