Hali ya Trump inaimarika,anaweza kurejea White House Jumatatu-Madaktari
Hali ya Rais wa Marekani Donald Trump inaimarika na anaweza kurejea katika Ikulu ya White House leo jumatatu madaktari wanaoongoza matibabu yake wamesema siku ya jumapili .
Ujumbe huoumetolewa baada ya msururu wa jumbe za kukinzana kuhusu hali ya rais Huyo aliyepatikana na virusi vya covid 19 na kusababisha mkanganyiko mkubwa kuhusu hali yake .
" Mgonjwa anaendelea kupata nafuu . amesalia bila homa kuanzia ijumaa na vungo vyake muhimu viko sawa’ amesema Dr. Sean Dooley katika hospitali ya kijeshi ya Walter Reed National Military Medical Center, ambako Trump amelazwa tangu siku ya ijumaa .
Trump alitoa video ya dakika nne siku ya jumamosi akisema ‘mtihani’ mkubwa wa hali yake utakuwa katika siku chache zijazo .
Utafiti wa kura ya maoni uliofanywa na A Reuters/Ipsos uliochapishwa jumapili umeonyesha kwamba Biden anamshindia Trump pengo la alama kumi kuliko ilivyokuwa hapo awali . Asilimia 65 ya wamerakani wansema Trumpo hangepatikana na virusi hivyo endapo angelichukulia janga la corona kwa uzito .