Hali ya Trump inaimarika,anaweza kurejea White House Jumatatu-Madaktari

Trump
Trump
Hali ya Rais wa Marekani Donald Trump  inaimarika na anaweza kurejea  katika Ikulu ya White House leo jumatatu  madaktari wanaoongoza matibabu yake wamesema siku ya jumapili .

Ujumbe huoumetolewa baada ya msururu wa jumbe za kukinzana kuhusu hali ya rais Huyo aliyepatikana na virusi vya covid 19 na kusababisha mkanganyiko mkubwa kuhusu hali yake .

" Mgonjwa anaendelea kupata nafuu . amesalia bila homa kuanzia ijumaa  na vungo vyake muhimu viko sawa’ amesema   Dr. Sean Dooley katika hospitali ya kijeshi ya   Walter Reed National Military Medical Center,  ambako Trump amelazwa tangu siku ya ijumaa .

Trump  alitoa video ya dakika nne siku ya jumamosi akisema ‘mtihani’ mkubwa wa hali yake utakuwa katika siku chache zijazo .

Utafiti wa kura ya maoni uliofanywa na A Reuters/Ipsos  uliochapishwa jumapili umeonyesha kwamba Biden anamshindia Trump pengo la  alama kumi  kuliko ilivyokuwa hapo awali . Asilimia 65 ya wamerakani wansema Trumpo hangepatikana na virusi hivyo endapo angelichukulia janga la corona kwa uzito .