Larry Madowo afichua mafuriko katika JKIA baada ya mvua kubwa kunyesha

Katika ripoti yake ya hivi punde, Madowo alishiriki video akifichua kiwango cha mafuriko katika eneo la mizigo la uwanja wa ndege wa JKIA.

Muhtasari
  • Kanda hiyo ilifichua maua mapya yaliyopakiwa, yakiwa yamehifadhiwa vizuri katika eneo la kuhifadhia baridi, sasa yakielea majini.
Larry Madowo,
Larry Madowo,
Image: HISANI

Madowo amekuwa akiangazia suala la paa zinazovuja katika JKIA wiki zilizopita, akimtaka Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen kuchukua hatua.

Katika ripoti yake ya hivi punde, Madowo alionyesha video akifichua kiwango cha mafuriko katika eneo la mizigo la uwanja wa ndege wa JKIA.

Kanda hiyo ilifichua maua mapya yaliyopakiwa, yakiwa yamehifadhiwa vizuri katika eneo la baridi, sasa yakielea majini.

Uharibifu huu ulisababishwa na mvua kubwa iliyonyesha Jumamosi usiku, Aprili 27.

Haya ni baadhi ya maoni kutoka kwa wanamitandao.

Bella@_Nana_Kc: What a loss.. So much for an international airport.. Damn!

Alex@iMuthembaa: You are embarrassing us jamani.

Super Marcus@noskyea:  Murkomen ni kama atatoka hii App

Amwoga Khalwale@amwogakhalwale: Terrible

victor machuka@mokayavic: Hapa ni insurance inagharamia ama

Brejin@Iambrejin: Ruto is doing a fine job,relax everything is in control.

𝔽𝕣𝕖𝕕 @AkangaFred: Are they still blaming the previous regime

Brejin@Iambrejin: UDA is the best governance this country has ever had,mmeona hadi dola imeshuka wangwana

Hivi majuzi alishambulia waziri wa Uchukuzi  Kipchumba Murkomen baada ya waziri huyo kumsuta kwa kutangaza suala la uvujaji wa paa katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Murkomen alielezea kutofurahishwa kwake na maoni ya Madowo ya kumshauri dhidi ya nchi yake katika hali mbaya.

Akitoa mfano wa matukio kadhaa, ikiwa ni pamoja na maoni ya awali ya Madowo kuhusu mafuriko kwenye barabara kuu ya Nairobi, Waziri huyo alimshutumu kwa kuendeleza mtazamo hasi kuhusu Kenya.

Waziri huyo pia alidai kuwa Madowo alianza kuibua wasiwasi huu ghafla baada ya kusafiri nje ya nchi.