Larry Madowo ashangaa kuuziwa ugali-omena shilingi 1200, “Kwani omena ilipewa heshima lini?”

Kwa kawaida katika migahawa mingi jijini Nairobi, ugali na omena huuzwa kwa shilingi 150 kwa sahani lakini Madowo japo hakutaja eneo alilokula chakula hicho, alionesha mshangao wake kuuziwa kwa shilingi 1,200.

Muhtasari

• “Chakula hiki kiligharimu KSh1,200. Kwani omena iliheshimiwa lini?” Madowo aliuliza na kuongeza, “Jee huu ni uungwana?”

Ugali na Omena
Ugali na Omena
Image: Facebook

Ripota wa CNN kuhusu masuala ya Afrika, Larry Madowo ameonyesha mshangao wake baada ya kudai kuuziwa msosi wa ugali na omena kwa Zaidi ya shilingi elfu moja pesa za Kenya.

Kwa kawaida katika migahawa mingi jijini Nairobi, ugali na omena huuzwa kwa shilingi 150 kwa sahani lakini Madowo japo hakutaja eneo alilokula chakula hicho, alionesha mshangao wake kuuziwa kwa shilingi 1,200.

Madowo aliuliza swali la balagha kutaka kujua ni tangu lini chakula aina ya dagaa kiliheshimishwa na kupandishwa hadhi ya kukifanya kuwa cha bei ghali, hali ya kuwa wengi wanakichukulia kuwa chakula cha kawaida na ambacho bei yake inastahili kuwa ya kawaida pia.

“Chakula hiki kiligharimu KSh1,200. Kwani omena iliheshimiwa lini?” Madowo aliuliza na kuongeza, “Jee huu ni uungwana?”

Kwenye upande wa maoni katika chapisho hilo kwenye Facebook, Madowo aliuliza bei halali ya chakula hicho na kushangaa hata Zaidi baadhi walipomwambia kwamba hakifai kuzidi shilingi 70 kwa sahani moja.

Haya hapa ni baadhi ya maoni;

“Miuse o funds buana...hii huku mtaa ni 70 🙄🤔😂😂..na unashiba mpaka supper” Baraza Fred.

“Je, huo ndio ugali na omena wa kawaida tunaowajua kweli?” Kereyian Meshack.

“Bro iyo doo yote?!.. acha ninunue bati tatu huku nijikaangie. 😂 Sikieni umaskini ikiongea sasa.” Sagini Ryans.

“Ni wewe uliyeenda kwenye hoteli ya nyota 5. Afadhali Omena/ugali pamoja na kipande cha limau huenda kwa Shilingi 200.🤣🤣🤣” Josephine Gathi.

Je, chakula cha ugali na omena kinakwenda kwa bei gani katika sehemu unayoijua?