“Bado nina muda!” Larry Madowo azungumzia ndoa baada ya bwenyenye Rupert Murdoch kuoa akiwa 92

Mwanahabari maarufu wa Kenya Larry Madowo amebainisha kuwa bado hajachelewa kufunga ndoa.

Muhtasari

•Madowo alisema bado ana muda wa kuoa kufuatia habari za mfanyabiashara tajiri Rupert Murdoch kufunga ndoa akiwa na umri wa miaka 92.

•Huenda huu ni uthibitisho kuwa mtangazaji huyo bado hajaoa licha ya kuhusishwa kimapenzi na mwanahabari mwenzake Edith Kimani

Larry Madowo na Edith Kimani
Image: INSTAGRAM// EDITH KIMANI

Huenda huu ni uthibitisho kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa NTV bado hajaoa licha ya kuhusishwa kimapenzi na mwanahabari mwenzake Edith Kimani

Mtangazaji huyo mashuhuri mwenye umri wa miaka 36 ambaye kwa sasa anafanya kazi katika CNN alisema kuwa bado ana muda wa kuoa kufuatia habari za mfanyabiashara tajiri Rupert Murdoch kufunga ndoa akiwa na umri wa miaka 92.

Madowo alichapisha screenshot ya kichwa cha habari cha ndoa ya Bw Murdoch na kunukuu, "Bado nina wakati."

Huenda huu ni uthibitisho kuwa mtangazaji huyo wa zamani wa NTV bado hajaoa licha ya kuhusishwa kimapenzi na mwanahabari mwenzake Edith Kimani.

Kwa muda mrefu, Wakenya wamekuwa wakidhani kwamba wawili hao wanachumbiana, kufuatia matendo yao ya wazi kwenye mitandao ya kijamii na matukio yao mazuri ya pamoja ambayo mara nyingi huwa wanashiriki hadharani.

Kuelekea mwishoni mwa mwezi Januari, Madowo aliamua kuwafanya mashabiki kukisia zaidi kwa ku-share post ambayo ilizidisha tetesi hizo kuwa yeye na Edith ni zaidi ya marafiki wa karibu.

Picha hiyo zuri iliambatana na nukuu fupi na tamu iliyosomeka, "Ikiwa sio hivi, sitaki📸 @gathigesest."

Na alichokuwa anakitaka Larry, ndicho alichokipata, kuzungumziwa. Chapisho hilo liliibua hisia mseto kutoka kwa mashabiki wake ambao waliamua kusherehekea 'uhusiano' kati ya nyota hao wawili wa habari.

Mapema mwaka jana, Edith alishiriki picha nzuri iliyoonyesha akimbusu Larry kwenye shavu lake na ujumbe mzuri kuhusu upendo wao kwa kila mmoja.

Edith alinukuu tukio hili,"Mwaka mpya. Same me. Bili sawa. Same love.@larrymadowo amechange wallet lakini, kwa hivyo matumizi mpya."

Wawili hao kwa muda mrefu wamekuwa wakidhaniwa kuwa wapenzi lakini hawakuwahi kuifanya rasmi.