Baadhi ya mambo ya kutatanisha ambayo Kanyari amefanya tangu kujiunga na TikTok

Amekuwa akijifunza mengi kutoka kwa wafuasi wake na kufahamiana na Tiktokers tofauti tangu alipojiunga na jukwaa hiyo.

Muhtasari
  • Kanyari alikanusha kwamba alifuata pesa kule na kusema kwamba lengo lake kuu ni kupeleka injili kwa vijana.
  • Kwenye mtandao huo, mchungaji huyo alifahamiana na Tiktoker anayejulikana kama Tizian, akimsifu kwa utanashati wake.
PASTA KANYARI VICTOR
PASTA KANYARI VICTOR
Image: HISANI

Nabii mwenye utata Victor Kanyari, alijiunga na TikTok hivi majuzi na amekuwa akifanya vipindi vya moja kwa moja, ambavyo vimekuwa vikimpatia umaarufu zaidi miongoni mwa manufaa mengine. 

Baada ya kujiunga kwenye mtandao huo wa video fupi, Kanyari alikanusha kwamba alifuata pesa kule na kusema kwamba lengo lake kuu ni kupeleka injili kwa vijana, ambao asilimia kubwa ndio wanaotumia mtandao huo

Amekuwa akijifunza mengi kutoka kwa wafuasi wake na kukutana na Tiktokers tofauti tangu alipojiunga na jukwaa hiyo.

Leo tutaangazia baadhi ya mambo ya kutatanisha Kanyari amefanya tangu alipojiunga na TikTok.

Katika kipindi cha moja kwa moja, Mchungaji Kanyari alinaswa kwenye video akiomba zawadi kwa njia isiyo ya kawaida, akisema,“Naskia hapa hawatumi sadaka, tumeni maua, tumeni Lion na mtume kofia”.

Ombi hili lisilotarajiwa imewaacha wengi wakikuna vichwa vyao na kutilia shaka nia ya maombi kama hayo.

Kwenye mtandao huo, mchungaji huyo alifahamiana na Tiktoker anayejulikana kama Tizian, akimsifu kwa utanashati wake akisema kwamba kijana huyo anamchochea kutaka kusuka nywele za rasta kama yeye na hata kuanza kuendesha pikipiki.

Akizungumza katika moja ya vipindi vyake vya moja kwa moja kwenye mtandao wa TikTok, Kanyari alisema kwamba yeye alipitia maisha ya mateso sana na sasa mahali amefikia hawezi kubali kuwa maskini kwa makusudi ili kuwafurahisha watu.

Baadhi ya wanamtandao pia hawakupendezwa na pastor huyo kuongea na Chokuu katika live yake ya TikTok lakini mhubiri huyo alionekana kutojali na kusema kuwa bado yeye ataendelea kuongea naye kama rafiki.

Hata hivyo, Kanyari alimpa changamoto Chokuu akitaka amfafanulie kauli yake kuwa yeye ni ‘chapati pendua’.

Alielezea wafuasi wake  awali alikuwa ameoa msanii wa injili Betty Bayo lakini baada ya kutengana, sasa anarudi sokoni na anatafuta mke, si kwingine bali TikTok.