“Hata dadangu ananichomea” Larry Madowo baada ya dadake kumuita ‘Mzee wa 50’

Kwa mujibu wa taarifa za kibinafsi za Madowo kwenye umma, mtangazaji huyo wa zamani wa NTV Kenya ana umri wa miaka 36.

Muhtasari

• “Hata dadangu ananichomea picha sasa,” huku akimalizia kwa emoji ya kucheka.

Larry Madowo,
Larry Madowo,
Image: HISANI

Larry Madowo, Mwandishi wa Habari wa Kimataifa wa CNN na mwenyeji wa kipindi cha African Voices Changemakers and Playmakers amedai kwa utani kwamba hata dadake mwenyewe sasa ameanza kumchomea picha kwa kumuita mzee wa miaka hamsini.

Kupitia Facebook yake, Madowo alipakia screenshot ya ujumbe aliomtumia Liz, ambaye alidai kuwa ni dadake.

 Ujumbe huo wa salamu ulisoma, “Habari yako mzee wa miaka 50” akimalizia na emoji ya kulia na nyingine ya kucheka.

Madowo alionekana kupatwa ghafla na ujumbe huo asioutarajia kutoka kwa dadake, alisema;

“Hata dadangu ananichomea picha sasa,” huku akimalizia kwa emoji ya kucheka.

Kwa mujibu wa taarifa za kibinafsi za Madowo kwenye umma, mtangazaji huyo wa zamani wa NTV Kenya ana umri wa miaka 36.

Hapo awali alikuwa Mwanahabari wa Amerika Kaskazini wa BBC na pia alitia nanga habari muhimu na akawasilisha BBC World News America kutoka Washington, DC.

Licha ya mafanikio mengi na makubwa kwenye tasnia ya uanahabari, Madowo anatajwa kuwa bado ni kapera.

Mtangazaji huyo wa CNN katika kipindi cha saa 24 zilizopita amekuwa akijibizana na waziri wa barabara na miundombinu, Kipchumba Murkomen kuhusiana na hali mbaya kwenye paa za majengo ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta.

Madowo alipakia video akionesha paa hizo zikivuja, jambo ambalo Murkomen aliona si sahihi, akidai kwamba Madowo anatumia vibaya umaarufu wake kimataifa.

Waziri huyo alimshauri Madowo kujaribu kuona na mazuri pia ambayo serikali ya Kenya imefanya ili kuyaweka kule nje, akisema kuendelea kuanika yale mabaya pekee ni kuchafua picha ya nchi kimataifa.