Ojaamong

Mahakama kuu imesimamisha kwa muda kesi ya ufisadi inayomhusu gavana wa Busia Sospeter Ojamoong   ya shilingi milioni nane

Jaji John Onyiego amesitisha kesi hiyo siku a jumatatu  baada ya Ojaamong kuwasilisha ombi akiwashtumu mashahidi wa upande wa mashtaka wa kumtishia .

Kesi hiyo imesitishwa hadi oktoba tarehe 12  ambapo mahakama itatoa maelekezo Zaidi .

Ojaamong  kupitia wakili  wake James Orengo   analishtumu kundi la  mashtaka likiongozwa na Taib Ali Taib kwa kuvuruga ushahidi na kuwatishia mashahidi wake .

Gavana huyo alifikishwa kortini mwaka wa 2018  kwa kutumia vibaya maamlaka ya afisi yake na mashtaka mengine kuhusiana na ufisadi .

Anashtumiwa wa kusaini makubaliano  na  Madam R Enterprises  Ltd  katika mradi wa ukusanyaji taka  bila kuzingatia sheria za usimamizi wa  raslimali za umma  na kusababisha kupotea shilingi milioni 8 pesa za umma . ameshtakiwa pamoja na  Madam R na maafisa wengine wa kaunti

Upande wa mashtaka  umewaita mashahidi 20  na kufunga kesi yake februari tarehe 20 mwaka huu .

View Comments