Jopo hilo litashughulikia kesi zote kuhusu kuvunjwa kwa bunge
Naibu Jaji Mkuu ateua jopo la majaji 5 kushughulikia kesi za kuvunjwa kwa bunge
Wabunge wamelaani ushauri wa Jaji mkuu kwa rais
- Jopo hilo litaongozwa na jaji Lydia Achode
- Majaji wengine ni George Odunga, James Makau, Anthony Ndungu na Pauline Nyamweya
Naibu Jaji mkuu Philomena Mwilu ameliteua jopo la majaji watano ili kuzisikiza kesi kuhusiana na ushauri wa jaji Mkuu kwa rais Uhuru Kenyatta kulivunja bunge.
Jopo hilo litaongozwa na jaji Lydia Achode.Majaji wengine ni George Odunga, James Makau, Anthony Ndungu na Pauline Nyamweya.
Kuna kesi sita kuhusu ushauri huo wa Maraga kwa rais Uhuru
Miongoni mwa kesi hizo ni ile ya wakenya wawili waliowasilisha ombi la kutaka mahakama kutupilia mbali ushauri wa jaji mkuu kwa rais. Bunge pia limemshtaki Jaji mkuu David Maraga na katika kesi nyingine Mwanasheria mkuu Kiharaka Kariuki amewasilisha ombi kupinga ushauri wa Jaji mkuu kuhusu kuvunjwa kwa bunge.
Bunge limesema kuvunjwa kwake sio jambo linalowezekana kama alivyoshauri jaji mkuu. Bunge limesema hatua hiyo ya Maraga ni kosa kubwa na halipo katika sheria.
Wabunge wanasema iwapo rais atafuata ushauri wa Maraga basi misuada yote iliyoidhinishwa na rais kuwa sheria kupitia wabunge haitaweza kutekelezwa kwa sheria.
Mwanasheria mkuu Kihara Kariuki naye amesema iwapo bunge litavunjwa hatua hiyo itampa rais Muhula mwingine.
Muungano wa Third Way Alliance nao pia una kesi ya kutaka mahakama itafisiri katiba kuhusu suala la kulivunja bunge.
Chama cha mawakili nchini LSK hata hivyo kinaunga mkono ushauri huo wa Maraga. Rais wa LSK Nelson Havi wiki hii aliongoza mawakili kulitwaa bunge akisema kwamba wabunge kwa sasa wanahudumu kinyume na sheria.