Maafisa wa polisi wa DCI asubuhi ya Jumanne,20,wamemtia mbaroni mshukiwa mmoja aliyetekeleza ubakaji, unajisi na mauaji eneo la Ruiru.
Levy Abubakara,36 alitekeleza kitendo hicho mnamo mwezi wa Oktoba ,16,2020 huku akiwa na wenzake wawili katika eneo la Membley kata ndogo ya Ruiru.
Levy alikamatwa baada ya maafisa hao kuchunguza kamera za siri ili kuchunguza kesi hiyo, mshukiwa huyo alionekana na wenzake wakiingia nyumbani humo na kumnajisi msichana wa miaka 16, na kisha wakambaka mfanyakazi kabla ya kumuua.