Jamaa aliyeshinda kesi ya mzozo wa ardhi na naibu rais William Ruto aliaga dunia mnamo JUmanne,27,Oktoba.
Kifo chake Adrian Gilbert Muteshi, 86, kilitangazwa na gazetti moja la humu nchini huku wakiandika ujumbe huu.
"Ni kwa hali ya kina na ya huzuni kutangaza kifo chake Adrian aliyeaga dunia akiwa mjini Nairobi." Baadhi ya tangazo hilo ilisoma.
Tangazo hilo halikutangaza kiini cha kifo cha mwendazake, jamaa na marafiki wanatarajiwa kukutana kuanzia Alhamisi wiki hii mwendo wa saa kumi na moja hadi saa moja usiku katika eneo la United Kenya Club.