In Summary
  • Moses Kuria kuwanai kiti cha ugavana Nairobi, ni habari ambazo zimesambaa sana kwenye mitandao ya kijamii
  • Hii ni baada ya Sonko kubanduliwa afisni na seneti wiki jana
  • JUmatatu spika wa bunge la Nairobi Mutura aliapishwa kushikilia wadhifa huo
Moses Kuria

Je Moses Kuria atajiuzulu na kuwania kiti cha ugavana Nairobi? ni swali ambalo limesalia vichwani vya wakenya baada habari kuenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa mbunge huyo wa Gatundu atajiuzulu na kuwania kiti cha ugavana.

Duru za habari ziliarifu kwamba Kuria alisema anataka kumrithi Sonko kama gavana wa jiji kupitia chama chake cha Peoples Empowerment Party.

Tayari tangazo la Kuria limeibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya mitandaoni.

 

"Kati ya Moses Kuria na Margaret Wanjiru ni nani anaweza kushinda kiti cha ugavana asubuhi na mapema?" aliuliza Wahome Thuku

Spika Benson Mutura aliapishwa Jumatatu Disemba 21 kushikilia wadhifa huo hadi uchaguzi mdogo ufanyike.

Sonko alitimuliwa Alhamisi Disemba 17 baada ya maseneta 27 kupiga kura ya kuunga mkono hatua ya MCAs kumbandua.

Alikosoa hatua hiyo na kusema iliingiliwa kisiasa na pia kudai maseneta walihongwa ili waunge mkono hoja ya kumtuma nyumbani.

Aidha gavana huyo ameelekea mahakamani kupinga kubanduliwa kwake.

Kulingana na seneta wa Narok Ledama Olekina Moses atajiuzulu endapo atashinda katia kinyang'anyiro cha ugavana.

View Comments