ULAGHAI MITANDAONI
Maelfu ya Wakenya walia kulaghaiwa mitandaoni
Wakenya wahofiwa kupoteza mamillioni waliowekeza kwenye mpango wa 'Amazon Web Worker'
•Mitandao ya kijamii ilitumika kama chambo cha kushawishi wengine kujiunga
•Wakenya walichukua mikopo ili kuwekeza
Kikundi kikubwa cha Wakenya kinalia kulaghaiwa baada ya kuwekeza kwenye mpango wa kimtandao uliojulikana kama 'Amazon Web Worker.'
Mpango huo ulikuwa umepata umaarafu mkubwa mno nchini huku maelfu ya Wakenya wakiabulia kwenye mtego huo ambao kwa sasa umetolewa kwenye programu ya Play Store. Maafisa waanzilishi walioonekana kusimamia shughuli hiyo pia hawapatikani tena tangu mwisho wa wiki iliyopita.
Hata hivyo, programu hiyo inadaiwa kutolewa kwenye programu ya Playstore na kisha maafisa wake kugura kutoka vikundi vilivyokuwa vinajumuisha waliokuwa wamejiunga na mpango huo mtandaoni.
"Amazon ni kesi iliyofungwa. Niko kwa vikundi zote na maafisa wote wamejitoa na kutungia njia zote za kuwafikia" Mtumizi wa Facebook kwa anayejitambulisha kama Lynne Mwangi aliandika kwenye kikundi cha AMAZON WEB WORKER KENYA kwenye mtandao huo wa Facebook
Waliokuwa kwenye mpango huo walikuwa wanatumia mitandao ya kijamii kujulishana na kushawishiana wenzao kujiunga wakiahidiwa utajiri mkubwa. Baadhi ya Wakenya waliendelea kutoa hisia zao na kukiri namna walikuwa wameanguka kwenye mtego huo laghai.
Hizi hapa baadhi ya hisia zilizotelewa na Wakenya kwenye mtandao wa Twitter.
Wamo baadhi ya waliojipata kwenye mpango wa Amazon wanaodai kuahidiwa kurejeshewa pesa zao mnao siku ya Jumanne na kwa sasa wanaishi kwa matarajio tu ila kulingana na Wakenya waliokuwa wamejipata kwenye ulaghai kama huo nafasi ya wao kupata pesa zao ni finyu sana.
Sio mara ya kwanza Wakenya wannajipata kwenye ulaghai mitandaoni kwani mara kwa mara mipango kama ile hujitokeza ikiwemo mmoja ambao uliwapata wengi mwakani 2017 ulitambulika kama ‘Public likes’