Babake mhasiriwa, Alfeus Ongou amesema kuwa binti yake alijaribu kueleza bwana yake kuwa walikuwa wakizungumza kuhusiana na masomo ya wanao watatu ila bwanake ambaye ni afisa pande hizo za Homabay hakutaka kuskia.
Hapo na hapo akaanza kumpiga kabla ya kumdunga kwenye sehemu zake za siri kwa kutumia kucha zake.
"Nahofia kwa kuwa binti yangu amedhulumiwa vibaya. Mpaka alimdunga kwa kucha zake. Nahofia huenda akamuua" Ongou alisema.
Kesi hiyo iliripotiwa katika kituo cha polisi cha Oyugis usiku huo kabla ya mhasiriwa kuenda kutibiwa katika hospitali ya Rachuonyo.
Naibu Kamishna wa kaunti, David Kiprop amelaani kitendo hicho na kukiita cha kikatili huku akiahidi kuwa mshukiwa atafunguliwa mashtaka punde baada ya kukamatwa.
Kiprop alisihi walio kwenye ndoa kusuluhisha migogoro yao kwa njia ambayo haisababishi madhara kama vile kuhusisha wazee wa kijiji na wataalam wa kushauriana kuhusu mambo ya ndoa.