In Summary

• Anataka mahakama kumlazimisha spika kuwa anampatia Sh200,000 kila mwezi  za kukimu mahitaji ya mtoto huyo ambaye hajazaliwa bado

•Alidai kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa huyo aliyekuwa gavana wa Bungoma kwa kipindi cha miaka mitatu na kutokana na uhusiano huo akapata mimba

Spika wa seneti Kenneth Lusaka
Image: MAKTABA

Mwanamke aliyedai kuwa mpango wa kando wa spika wa seneti Kenneth Lusaka anataka shilingi milioni 25 kutoka kwake ili kugharamia mahitaji ya mtoto ambaye amebeba.

Mwanamke huyo ambaye alifika mahakamani siku ya Jumatatu na kudai kuwa mimba aliyokuwa amebeba ni ya Lusaka anataka mahakama kumlazimisha spika kuwa anampatia Sh200,000 kila mwezi  za kukimu mahitaji ya mtoto huyo ambaye hajazaliwa bado

Alidai kuwa amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanasiasa huyo aliyekuwa gavana wa Bungoma kwa kipindi cha miaka mitatu na kutokana na uhusiano huo akapata mimba.

Wakili wa mlalamishi, Danstan Omari ameomba mahakama kuagiza Lusaka kukubali majukumu ya mtoto huyo. Alimtaka spika kugharamia bili zote za kliniki na hospitali katika ujauzito wa mlalamishi.

Mlalamishi alisema kuwa Lusaka alikuwa amekanusha uhusiano wowote na mimba ambayo alikuwa amebeba licha ya kujua kuwa walikuwa wakishiriki tendo la ndoa bila kinga.

Jaji James Makau alifanya dharura kesi hiyo siku ya Jumatatu na kuagiza isikizwe mnamo Julai 7.

View Comments