In Summary

•Lotada Loyara aliaga papo hapo ilhali bibi yake alikata roho alipokuwa anakimbizwa katika hospitali ya Chemoling'ot iliyo umbali wa takriban kilomita 50 kutokana na jereha mbaya ya risasi tumboni. Mtoto wao wa miaka miwili , Musto Lotada, aliachwa na majeraha mabaya.

•Mjumbe wa wadi ya Tiriko, Sam Lokales alisema kuwa familia hiyo ilikuwa imelala mida ya saa tisa asubuhi wakati magaidi hao waliwavamia na kumiminia risasi.

Mutso Lotada wa miaka miwili akiwa hospitalini ya Chemolingot siku ya Jumatano
Image: Joseph Kangogo

Hali ya hofu imetanda katika kijiji cha Kapau maeneo ya Tiaty, kaunti ya Baringo baada ya magaidi kuvamia boma moja na kuua wanandoa na kujeruhi mtoto wao asubuhi ya kuamkia Jumatano.

Lotada Loyara aliaga papo hapo ilhali bibi yake alikata roho alipokuwa anakimbizwa katika hospitali ya Chemoling'ot iliyo umbali wa takriban kilomita 50 kutokana na jereha mbaya ya risasi tumboni. Mtoto wao wa miaka miwili , Musto Lotada, aliachwa na majeraha mabaya.

Alipokuwa anathibitisha tukio hilo, naibu kamishna wa kaunti wa Tiaty ya Magharibi, Jackson Orieny alisemakuwa wanandoa waliaga wakati mtoto wao  aliugua majeraha kichwani na kwenye mkono wake wa kulia.

"Bado haijabainika wazi nia ya mashambulio hayo kwa hivyo sina habari kamili" Orieny alisema.

Alisema kuwa mashambulio ya mara kwa mara kati ya majirani katika maeneo hayo huenda yanachangiwa na kiangazi ambacho kimekithiri pale na kusababisha uhaba wa maji na chakula ya mifugo.

Mjumbe wa wadi ya Tiriko, Sam Lokales alisema kuwa familia hiyo ilikuwa imelala mida ya saa tisa asubuhi wakati magaidi hao waliwavamia na kumiminia risasi.

Daniel Tuwit akihutubia wanahabari
Image: Joseph Kangogo

Lokales na mwenzake wa wadi ya Ripko-Kositei, Daniel Tuwit walilaani kitendo hicho na kusema hakuna mifugo wowote ambao waliibiwa  kwenye uvamizi huo.

Wawili hao wamesihi serikali kupeleka maafisa wa kulinda usalama katika maeneo hayo ili kuimarisha amanina kuzuia mashambulio yanayoaminika kutoka maeneo ya Lomelo, kaunti jirani ya Turkana.

Mauaji haya yanajiri wakati operesheni ya kurejesha amani inaendelea maeneo ya Kapedo na Tiaty . Maafisa wa usalama wanatia juhudi kuwawinda magaidi ambao wamekuwa wakinyanyasa wakazi wa maeneo hayo.

View Comments