In Summary

•Hakimu mkuu, James Mwaniki, alimpata Jeremiah Mutinda na hatia kwa kitendo ambacho alitekeleza mnamo Machi 16 katika kijiji cha Kinze, Makueni.

•Mahakama ilimuonya mshtakiwa dhidi ya kutumia vileo kwa kukithiri.

court

Mwanaume mmoja kutoka Makueni ameagizwa na mahakama kufanya huduma ya jamii kwa miezi tisa baada ya kupatikana na hatia ya kutishia kuua mama yake.

Hakimu mkuu, James Mwaniki, alimpata Jeremiah Mutinda na hatia kwa kitendo ambacho alitekeleza mnamo Machi 16 katika kijiji cha Kinze, Makueni.

Inadaiwa kuwa Mutinda akiwa amejihami na panga alitishia kuua mamake, Martha Mwelu baada ya kuzozania mahari iliyotolewa dadake mdogo.

Mutinda alitaka kununua pikipiki na mgao wa pesa ambao angepata.

Upande wa mashtaka ulisema kuwa Mutinda na mama yake wamekuwa wakizozona mara kwa mara tangu mwaka wa 2007.

Afisa wa majaribio, Rose Malewa alikuwa amependekeza Mutinda apatiwe kifungo cha nyumbani kwani ilikuwa mara yake ya kwanza kufikishwa mahakamani na alikuwa mlevi wakati alitishia kuua mama yake.

Mahakama ilimuonya mshtakiwa dhidi ya kutumia vileo kwa kukithiri.

View Comments