In Summary

•Charles Mwenda kutoka Meru nchini Kenya alikuwa amefiwa na mkewe na alichotaka ni kuufikisha mwili wake nyumbani kwa mazishi 

•Jaji Edward Muriithi wa mahakama kuu ya Meru akitoa agizo hilo la kufidiwa kwa mlalamishi akisema jumatano kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi walipomkamata Mwenda mwenye umri wa miaka 32 na kwamba vitendo vyao havikuwa vya kiutu .

Image: Hisani

Picha yake akiwa amelala kando ya jeneza la mkewe iliwafanya watu wengi kutamaushwa na ukatili wa polisi.

Charles Mwenda kutoka Meru alikuwa amefiwa na mkewe na alichotaka ni kuufikisha mwili wake nyumbani kwa mazishi .

Lakini polisi hawakumruhusu kufanya hivyo kwa sababu muda wa watu kusafiri ulikuwa umekwisha kwa mujibu wa masharti ya kupambana na janga la Corona mwaka jana .

Hatimaye mahakama imeagiza afidiwe shilingi milioni 1.5 kwa masaibu yake na jinsi alivyoteseka wakati wa kipindi hicho na hata kunyeshewa na mvua akiwarai polisi kumruhusu akamilishe safari ya kuufikisha nyumbani mwili wa mke wake .

Mwenda alilazimika kulala na mwili wa mke wake nje ya kituo cha polisi .

Jaji Edward Muriithi wa mahakama kuu ya Meru akitoa agizo hilo la kufidiwa kwa mlalamishi akisema jumatano kwamba polisi walitumia nguvu kupita kiasi walipomkamata Mwenda mwenye umri wa miaka 32 na kwamba vitendo vyao havikuwa vya kiutu .

Jaji alisema kwamba haki za Mwenda zilivunjwa na polisi ndio wanaofaa kuwajibikia vitendo vyao .

Amemuagiza Inspekta mkuu wa polisi kusimamia gharama hiyo .

Mwenda pamoja na waombolezaji wengine 31 walikuwa wamesafiri kutoka Malindi ,Pwani mwa Kenya hadi Meru- eneo la Kati mwa nchi hiyo tarehe 28 Mei mwaka jana kumzika mkewe Faith Mwende ambaye aliaga dunia baada ya kuugua saratani.

Walisimamishwa na polisi kilomita chache kutoka nyumbani kwake ambapo mazishi yalifaa kufanyika na kuagizwa kurejea Malindi walikokuwa wametoka.

View Comments