Watu 5 wakamatwa wakijaribu kuiba benki ya Prime Nairobi
- Watu 5 wakamatwa wakijaribu kuiba benki ya Prime Nairobi
- Hata hivyo wapelelezi walifahamishwa kuhusu mpango wa wahalifu hao na kuwafumania
Watuhumiwa watano wamematwa wakati walipokuwa wakijaribu kuiba kutoka kwa benki ya Prime katika Wilaya ya Biashara ya Kati ya Nairobi (CBD) Ijumaa, Julai 2.
Kulingana na DCI maafisa wa polisi waliambiwa kuwa watuhumiwa walikuwa wamekomboa nyumba katika vyumba vya wageni Angle House barabara ya Ukwala.
"kundi la wahalifu watano walioshukiwa kuwa na mpango wa kuvunja benki ya Prime Bank OTC, walikamatwa mapema leo asubuhi. Charles Mulo, Fredrick Muuderwa, Jesse Muriuki, Gabriel Mungai na Reuben Njuka walikamatwa na timu ya polisi kutoka kituo cha polisi cha DCI na Kamukunji,"DCI Ilisema.
Hata hivyo wapelelezi walifahamishwa kuhusu mpango wa wahalifu hao na kuwafumania na kuharibu mpango wao.
Watuhumiwa hao walipelekwa katika kituo cha polisi cha Kamukunji huku waisubiri kufikishwa mahakamni.