In Summary

•Alipokuwa anahutubia wakazi wa Tana River mapema wiki hii, mbunge huyo wa Suna Mashariki aliwaomba Wakenya kutokubali viongozi ambao wanatoa ahadi ya kesho ilhali wana uwezo wa kuyatimiza kwa sasa.

•Mbunge huyo pia alikosoa mpango wa wanasiasa wanaounga naibu rais mkono wa kupatia vijana toroli akidai kuwa hazisaidii kutatua shida za Wakenya. Alisema kuwa siasa zao ni za kuwahadaa Wakenya.

JUNET.jfif

Kiongozi wa walio wachache bungeni Junet Mohamed ametia doa kampeni za naibu rais William Ruto za kuwania urais mwaka ujao akisema kuwa anawapa Wakenya ahadi anazoweza kutimiza kwa sasa.

Junet amepuuzilia mbali ahadi ambazo Ruto anawapa Wakenya akidai kuwa iwapo kweli ana nia  yuko katika nafasi  ya kutimiza anayoyahidi kwa sasa kuona kuwa yuko serikalini tayari.

Alipokuwa anahutubia wakazi wa Tana River mapema wiki hii, mbunge huyo wa Suna Mashariki aliwaomba Wakenya kutokubali viongozi ambao wanatoa ahadi ya kesho ilhali wana uwezo wa kuyatimiza kwa sasa.

"Watu ambao wako ndani ya serikali wanakuja hapa na kuwaambia eti ukinichagua nitakufanyia hii na hii na hii. Swali ambalo mnafaa muwaulize ni mbona usifanye hayo saa hizi? Si uko serikalini? Mbona unangoja tukuchague ndio ufanye?.. ni lazima mtu afanye kile anachoweza kwa sasa"  Junet alisema.

Mbunge huyo pia alikosoa mpango wa wanasiasa wanaounga naibu rais mkono wa kupatia vijana toroli akidai kuwa hazisaidii kutatua shida za Wakenya. Alisema kuwa siasa zao ni za kuwahadaa Wakenya.

"Wanatembea na pesa ambayo wamepora ndio wanataka kununua nayo wananchi. Wanakuja hapa na mambo ya Wheelbarrow ambayo hayawezi kusaidia Wakenya" Alidai Junet.

Alisema kuwa lengo kuu la chama cha ODM  iwapo watatwaa uongozi ni kuimarisha uchumi wa Kenya na kuleta pesa mifukoni mwa Wananchi.

"Sisi kama ODM tumejipanga na tunajua mwelekeo wetu. Lakini wale watu ambao wanakuja hapa kudanganya wananchi wakitumia umaskini kama silaha na kuwaambia lazima ubaki maskini ubaki hustler ndo akusaidie ni watu amabo wanakuja kuharibu uchumi wa Kenya. Lazima tujitenge na wao tubaki ODM" Junet alisema. 

Junet alitupilia mbali mfumo wa uchumi wa 'bottom up' ambao naibu rais anaahidi Wakenya na kusema kuwa mfumo wa ODM ikiongozwa na Raila Odinga  ni bora.

View Comments