In Summary

•Polisi maeneo ya Makueni wanazuilia mwanamke mmoja ili kusaidia katika upelelezi wa mauaji ya mumewe aliyetoweka siku kadhaa zilizopita.

•Kulingana na rekodi za polisi jembe na tupa ya kunolea vifaa zilizokuwa na damu pia zilipatikana kwenye eneo la tukio.

POLICE CRIME SCENE

Habari na Patrick Nyakundi

Polisi maeneo ya Makueni wanazuilia mwanamke mmoja ili kusaidia katika upelelezi wa mauaji ya mumewe aliyetoweka siku kadhaa zilizopita.

Purity Nzilani Mutindi alikamatwa baada ya matone ya damu kupatikana yamefululiza kutoka kichakani ambapo fuvu la kichwa, viungo vingine vya mwili na nguo za marehemu Reuben Mutisya Mwau zilipatikana hadi nyumbani kwake.

Kulingana na rekodi za polisi jembe, tupa ya kunolea vifaa zilizokuwa na damu pia zilipatikana kwenye eneo la tukio.

Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa polisi maeneo ya Makueni Joseph Ole Naipeyan alisema kuwa hakuna ripoti ilikuwa imepigwa kwamba marehemu alikuwa ametoweka.

"Marehemu aliuliwa nyumbani kwane kabla ya kutupwa. Viungo vyake vingine havijapatikana bado" Bw Naipeyan alisema mnamo Jumapili.

Mabaki ya mwili wa marehemu yaliyopatikana yalipelekwa katika mochari ya Kilungu huku upasuaji wa mwili ukisubiriwa.

View Comments