In Summary
  • Rais wa zamani wa Afrika Kusini FW de Klerk afariki akiwa na umri wa miaka 85
FW de Klerk
Image: Hisani

FW de Klerk, rais wa zamani wa Afrika Kusini na mzungu wa mwisho kuiongoza nchi hiyo, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85.

Bw de Klerk, ambaye pia alikuwa mhusika mkuu katika kipindi cha mpito cha taifa kuelekea demokrasia, alikuwa amepatikana na saratani mwaka huu, kulinagana na msemaji.

Bw de Klerk alikuwa mkuu wa nchi kati ya Septemba 1989 na Mei 1994.

Mwaka 1990 alitangaza kumwachilia huru kiongozi aliyepinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela, na kusababisha kura za vyama vingi mwaka 1994.

FW de Klerk
Image: Hisani
View Comments