Aliyekuwa Mkuu wa magereza Wycliffe Ogalo na Mkuu wa Gereza la Kamiti Charles Mutembei watiwa mbaroni
- Aliyekuwa Mkuu wa magereza Wycliffe Ogalo na Mkuu wa Gereza la Kamiti Charles Mutembei watiwa mbaroni
Kamishna Mkuu wa Magereza ya Kenya Wycliffe Ogalo na Mkuu wa Gereza la Kamiti Charles Mutembei wamekamatwa na maafisa wa upelelezi wa DCI.
Kukamatwa kwa wawili hao kunakuja muda mfupi baada ya Rais Uhuru Kenyatta kubatilisha uteuzi wa Ogalo kama Kamishna Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Kenya.
Nafasi yake ilichukuliwa na Brigedia mstaafu John Warioba ambaye aliapishwa mara moja.
Mabadiliko hayo yanafuatia kutoroka kwa hivi majuzi kwa wafungwa watatu wa ugaidi katika gereza la Kamiti Maximum.
"Mheshimiwa Rais leo amemteua na kushuhudia kuapishwa kwa Brigedia (Mst) John Kibaso Warioba kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza," taarifa kutoka Ikulu ilisema.
Waliotoroka ni pamoja na Mohamed Ali Abikar, ambaye alihukumiwa kwa jukumu lake katika shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa 2015 ambapo watu 148 waliuawa.
Mtu wa pili alikamatwa mwaka wa 2012 kutokana na shambulio lililozuiwa dhidi ya bunge la Kenya na wa tatu kwa kujaribu kujiunga na kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia.
The video could not be loaded.