In Summary

• Kainerugaba aliteuliwa tena kama Kamanda wa Kamandi ya Kikosi Maalum cha wasomi (SFC) mnamo 2020.

• Pia alikuwa amehudumu katika wadhifa huo kuanzia 2008 hadi 2017

Former Lt Gen Muhoozi Kainerugaba was the first senior military officer in Africa to come out on Russia's side.
Image: Getty Images

Muhoozi Kainerugaba, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni ametangaza kustaafu kama Mkuu wa Majeshi ya Nchi Kavu.

Kupitia akaunti yake rasmi ya Twitter, kijana huyo mwenye umri wa miaka 47 alisema kuwa amepata mafanikio mengi katika jeshi tangu achukue hatamu.

"Baada ya miaka 28 ya utumishi katika jeshi langu tukufu, jeshi kubwa zaidi duniani, nina furaha kutangaza kustaafu. Mimi na askari wangu tumefanikiwa sana!" Kainerugaba alisema.

Amekuwa kwenye vikosi kwa miaka 28 iliyopita." Nina upendo na heshima tu kwa wanaume na wanawake wote wakuu ambao wanafanikisha ukuu kwa Uganda kila siku."

Kainerugaba aliteuliwa tena kama Kamanda wa Kamandi ya Kikosi Maalum cha wasomi (SFC) mnamo 2020.

Pia alikuwa amehudumu katika nafasi hiyo hiyo kuanzia 2008 hadi 2017.

Kainerugaba  amegonga vichwa vya habari kwa siku za hivi karibuni baada ya kutoa maoni yake kuhusu mzozo wa Ukraine na Urusi.

Mnamo mwaka wa 2017, Muhoozi aliteuliwa kuwa Mshauri wa Rais, hatua iliyozua minong'ono tofauti kutoka kwa Waganda huku wengine wakisema kwamba alikuwa akiandaliwa kwa ajili ya urais.

 

View Comments