In Summary

•Bei mpya zitaanza kutumika saa sita usiku wa Alhamisi, Aprili 14 hadi saa sita usiku wa Mei 14, 2022.

•CEO wa EPRA Daniel Kiptoo alisema bei hizo mpya zinajumuisha VAT ya 8% kwa mujibu wa sheria ya Ushuru.

Petrol
Image: MAKTABA

Bei ya mafuta imeongezwa kwa Ksh9.90 katika tathmini ya mwezi Aprili ya Mamlaka ya Uthibiti wa Kawi (EPRA).

Hii inaaminisha lita moja ya petroli jijini Nairobi imepanda kutoka Ksh134.62 hadi Sh144.72.

Lita moja ya dizeli sasa itauzwa Ksh 125.50 kutoka Sh115.60.

Mafuta taa itauzwa shilingi 113. 44 jijini Nairobi kutoka Sh 103.54.

Bei mpya zitaanza kutumika saa sita usiku wa Alhamisi, Aprili 14 hadi saa sita usiku wa Mei 14, 2022.

Akitoa bei hizo mpya Alhamisi, CEO wa EPRA Daniel Kiptoo alisema bei hizo mpya zinajumuisha VAT ya 8% kwa mujibu wa sheria ya Ushuru.

Kiptoo alisema kupanda kwa bei hiyo kunatokana na ongezeko la 20.47% la wastani wa gharama ya kusafirisha mafuta ya petroli,  24.7% kwa  dizeli na 11.84% kwa  mafuta taa.

Hii inamaanisha mabadiliko ya 20.47% kwa gharama ya petroli, asilimia 24.7 kwa gharama ya dizeli na asilimia 11.84 kwa gharama ya mafuta ya taa.

Kwingineko, serikali imetangaza kuwachukulia hatua kali wafanyibiashara wa mafuta waliosababisha uhaba wa bidhaa hiyo nchini makusudi.

Akihutubia mkao wa wanahabari siku ya Alhamisi Kaimu waziri wa kawi Monica Juma pia aliwahakikishia wakenya kuwa mikakati imewekwa kuhakikisha kuwa hali ya kawaida inarejea katika muda wa saa 72.

Waziri alisema kwamba kunahifadhi ya kutosha ya mafuta nchini.

Alitowa wito kwa wananchi kuwa watulivu huku swala hilo likishughulikiwa.

Juma alishtumu vikali baadhi ya kampuni za mafuta nchini kwa kusababisha uhaba wa bidhaa ya mafuta nchini makusudi kwa manufaa yao ya binafsi.

 Waziri alisema alithibitisha kuwa nchi ina akiba ya mafuta ya kutosha ingawa alishtumu baadhi ya kampuni kwa kuficha mafuta na kuelekeza mgao wa mafuta yaliyonuiwa kwa soko la Kenya hadi nchi zingine katika kanda hii.

Alisema kuwa Mamlaka ya Nishati na Petroli na Udhibiti wa nishati tayari imetoa barua za kuonya kampuni za mafuta ili kusubiri kupandishwa kwa bei za bei katika bei mpya za kila mwezi.

Wenye magari pia wamehimizwa kuepuka kununua kiasi kikubwa cha mafuta ili kuepusha mzozo zaidi.

View Comments