In Summary

 

  •  Daktari wa Trump amesema hawezi kuambukizwa watu covid 19
  •  Rais Huyo amekataa kufanya mdahalo kupitia njia ya mtandao na mpinzani wake Biden 

 

Rais wa Marekani Donal Trump,akiitupa maski yake katika mkutano wa kampeini Florida

 

Rais wa Marekani amerejea tena katika kampeini chini ya wiki mbili tangu  alipopatikana na virusi vya corona .

 Maelfu walikuwanyika katika mkutano wake huko Sanford  ,Florida  ambako Trump alifanya mkutano mmoja kati ya msururu wa mikutano mine ya kampoeini  anapolenga kukitetea kiti chake katika uchaguzi wa tarehe 3 Novemba

 Siku ya jumatatu mpinzani wa Trump Joe Biden alikuwa katika jimbo la Ohio mbalo linatajwa kuwa muhimu kwa yeyote anayelenga kukishinda kiti hicho .

 Kura ya  maoni  inaonyesha kwamba Biden ameunda pengo la alama kumi na Bwana Trump .

 Baadhi ya majimbo ni muhimu sana kwani ndio yenye  usahuwisho kuhusu kura za wajumbe 270 ambazo mtu anahitaji ili kukinyakuwa kiti cha urais .

 Trump alipatikana na virusi vya corona siku 11  zilizopita na kulazwa hospitalini  siku moja baadaye . Siku ya jumapili daktari wake  alisema Trumo amepona virusi hivyo na hayupo katika hatari ya kuwaambukiza watu wengine .

 Kundi lake la kampeini limeamua kuingia Florida kwa  kishindo kwa sababu akizpoteza kura za eneo hilo huenda akapata ugumu wa kurejea White House .

 

View Comments