In Summary

 

  • Trump amesema hali yake imeboreka ingawaje haijulikanai iwapo amepona
  •    Rais huyo amekuwa akitibiwa katika hospitali moja ya kijeshi

 

Mgombeaji wa Urais wa chama cha Democrat Joe Biden

 

 Mgombeaji wa rais wa marekani wa tiketi  ya chama cha democrat  Joe Biden amesema hapafai kuwa na awmau ya pili ya mdahjalo wa urais iwapo rais Donald Trum bado hajapona virusi vya corona .

" Nafikiri bado anaugua covid 19 ,hatufai kuwa na mjadala huo’ Biden amesema siku ya jumanne

 

" Nafikiri itatulazimu kufuata kanuni kali .watu wengi wameambukizwa na hili ni tatizo kubw’

Mjadala huo wa  wagombeaji wa urais ulifaa kufanyika oktoba tarehe 15 Miami Florida

Trump  alipatikana na virusi vya corona tarehe 1 oktoba  lakini haijulikani aliambukizwa lini ugonjwa huo

Trump na Biden katika Mdahalo wa kwanza wa wagombea urais Marekani

 Kulingana na mwongozo wa   kiafya nchini Marekani Trump anafaa kujitenga kwa siku 10  tangu siku anayoaanza kuona daalili za ugonjwa huo . Matamshi ya Biden yanajiri baada ya kuibuka ripoti kwamba ugonjwa huo unasambaa kwa haraka miongoni mwa  watu wanaokaribiana na Trump  huku afisa moja wa kijeshi akiambukizwa pamoja na mshauri wa rais  Stephen Miller .

 Bwana  Miller, ambaye amejitenga kwa siku tano sasa amethibitisha kwamba aliambukizwa virusi hivyo siku ya jumanne .

 Jenerali mmoja wa kijeshi  Mark Milley  na viongozi wengine wa  jeshi pia wapo katika karantini  baada ya  afisa wa  kikosi cha ulinzi cha  Coast Guard Admiral Charles Ray  kupatikana na virusi hivyo .

 

View Comments