In Summary

• Watoto wapatao 25 wenye umri kati ya miaka mitano na sita wamefariki baada ya darasa lao kuungua moto.

• Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika bado.

• Masomo yamesitishwa katika shule hiyo kwa muda.

Image: Getty Images

Watoto wapatao 25 wenye umri kati ya miaka mitano na sita wamefariki baada ya darasa lao kuungua moto.

Wengine kadhaa walijeruhiwa wakati wa ajali hiyo ya moto ambayo ilitokea Jumatatu asubuhi wakati watoto wakiwa darasani wakisoma katika shule iliyopo eneo la Maradi.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika bado.

Nchini Niger, madarasa huwa yanajaa na mara nyingi hujengwa kwa kutumia mbao na majani wakati miundo mikuu ya matofali haiwezi kujenga shule zote.

Moto uliotokea Jumatatu umeteketeza madarasa matatu, meya wa mji wa Maradi, Chaibou Aboubacar, ameviambia vyombo vya habari.

Shuhuda mmoja ameiambia BBC kuwa ameona watoto kadhaa wakitolewa eneo la tukio na kupelekwa hospitali wakiwa katika hali ya mahututi.

Masomo yamesitishwa katika shule hiyo kwa muda.

Si kawaida kwa shule za Niger kuungua na kusababisha idadi kubwa ya vifo.

Ingawa mwanzoni mwa mwaka huu katika mji mkuu wa nchi hiyo shule iliungua na kuua watoto 20 .

View Comments