In Summary

• Benedict amekuwa akisifiwa na wahafidhina wengi kwa misimamo yake mikal idhidi ya mapenzi ya jinsia moja katika kanisa.

• Kwa upande mwingine, wahafidhina hao wamekuwa wakimlaumu Francis kwa kauli zake zinazoashiria kukaribisha mapenzi ya jinsia moja katika kanisa.

Papa Benedict wakiwa na mrithi wake Papa Francis
Image: Maktaba

Majarida ya kimataifa yamemnukuu Papa Francisco wa kanisa Katoliki akitoa wito kwa kanisa na ulimwengu mzima kwa jumla kumweka kwenye maombi mtangulizi wake Papa Benedicto wa 16 ambaye ni mgonjwa sana.

Katika taarifa rasmi iliyotolewa na Papa Francis kutoka Vatican na ambayo ilipeperushwa moja kwqa moja kwa njia ya video, alisema kuwa anawaomba wote wenye moyo wa huruma kumkumbuka Benedicto wa 16 katika maombi maalum kwani ni ‘mgonjwa sana’.

"Ningependa kuwaomba nyote sala maalum kwa ajili ya Papa Mstaafu Benedict, ambaye, kwa ukimya, analitegemeza Kanisa. Tumkumbuke. Yeye ni mgonjwa sana, akimwomba Bwana amfariji na kumtegemeza katika ushuhuda huu wa upendo kwa Kanisa, hadi mwisho" Francis alisema katika tangazo la mshangao la Jumatano lililotolewa mwishoni mwa hadhira yake kuu ya kila wiki.

Taarifa ya Vatican ilisema Benedict alikuwa akipatiwa matibabu mara kwa mara na hali yake imedhibitiwa.

Papa wa zamani Benedict mwenye umri wa miaka 95, ni shujaa wa Wakatoliki wenye imani kali na ambaye mwaka 2013 alikuwa papa wa kwanza katika kipindi cha miaka 600 kujiuzulu.

Francis, ambaye alimtembelea papa huyo wa zamani baada ya kutoa tangazo hilo, mara nyingi amemsifu Benedict, akisema ni kama kuwa na babu nyumbani.

Kinyume na Benedicto wa 16 ambaye alikuwa na misimamo mikali dhidi ya mapenzi ya jinsia moja, mrithi wake Papa Francisco katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akinukuliwa kwa njia mbalimbali akionekana kukaribisha suala la mapenzi ya jinsia moja katika kanisa.

View Comments