In Summary

Tunakaribia mwaka mzima tangu kuripotiwa kwa  kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya korona humu nchini.

 

Huku siasa zikishika kasi, na  mambo kuchacha katika kaunti mbali mbali, kwasababu ya kura ya maamuzi. Masuala mengi yanayotukumba kama nchi yametupilwa mbali na kupewa mkono wa sahau . Vijana na masuala yetu yamewekwa kando, nafasi za kazi bado hazijabuniwa na hata walio chuoni shida zingalipo.

Tunakaribia mwaka mzima tangu kuripotiwa kwa  kisa cha kwanza cha maambukizi ya virusi vya korona humu nchini. Mambo yalibadilikakwa haraka na shule nyingi kufungwa . Mambo bado chuoni ni vile vile tangu wakati huo. Kama mwanafunzi nimelazimika kusomea mtandaoni sasa waelekea mwaka .

Nimeanza mhula mpya wiki hii tu na bado nasomea mtandaoni. Bado tunaendelea kuskia misuada kuhusu curfew na mambo mengineyo kuhusu janga hili. Swali kubwa kabisa kwetu ni jeh ugonjwa huu upo tu miongoni mwetu sisi wananchi sio wanasiasa . Huku nikilazimika kuhudhuria shule mtandaoni baada ya mwaka mmoja , wanasiasa wanhudhuria mikutano na  kukutana na wanachi wanvyotaka bila hata barakoa .

 

Katika mwanzo wa masomo haya ya mtandaoni, vyuo viliahidi kutupa jinsi ya kugharamia masomo haya, kutoka kwa  kununua kadi za simu na kupata ‘bundles’ mle ndani za kuhudhuria darasa hizi. Kwa sasa vyuo vimetuacha kujigharamia masomo haya . Kuongeza chumvi katika donda bado karo ikiwa ile ile .

Wanaofaidika ni vyuoni ilhali sisi kama wanafunzi tunaumia . Masomo yamekuwa biashara ya kupata faida huku wanafunzi na wazazi wao kuumia. Vyuo vinapata kuweka pesa mingi ya matumizi kwa sababu wanafunzi hawapo shuleni ,huku bado wanalipa karo za juu. Bajeti ikiwa ile ile lakini matumizi yamepungua, pia wamejiondelea jukumu la kusaidia wanafunzi kupata kuhudhuria masomo ya mitandaoni , na kuwachia wazazi.

Suala hili ni suala nyeti ambalo linafaa kushugulikiwa kabla wanafunzi na wazazi hawaja kandamzwa kwa muda mrefu. Mwaka mpya wa vyuo waanza na tumeachiwa kujikimu kwa vyovyote vile , huku pia tukilipa karo za juu. Wanasiasa wanakubaliwa kuwa na umati wa watu kubwa kuliko tulivyo chuoni, wanafunzi wa shule za chekechea wapo shuleni , hata wale wa shule za msingi na upili pia wapo shule , lakini wa vyuoni bado janga linagonga sana kwetu kurudi kwa urahisi. Nina uhakika kuwa kama motto wa shule ya chekechea anaaminiwa na serikali kujikinga na kuwakinga wenzake dhidhi ya korona hata wa chuo kikuu anauwezo huo.

Masomo ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya mwanadamu yeyote yule, na kama viongozi,wahandisi,wanahabari,madaktari ,wanahesabu  wa kesho tunahitaji masomo haya. Sio kukandamizwa na kulazimshwa kugharamia pakubwa hivi ili kupata elimu. Vyuo viache kutengeneza faida kutoka kwa kuwa vunja wanafunzi na wazazi miongongo, tushirikiana na tusaidiane ili tuimarishe kesho yetu na kesho ya Kenya.

View Comments