Maelezo kamili yanapaswa kuthibitishwa kabla ya mwisho wa Oktoba.Chama cha madaktari nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni kimeibua wasiwasi kuhusu kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kati ya madaktari na wauguzi nchini humo.
Makubaliano na Uingereza yanaweza kuwavutia wafanyikazi wengi wa huduma ya afya nchini Kenya kwani wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya kufanya kazi, malipo duni na hata kufanya kazi kwa miezi bila malipo.
Lakini kuna hofu kwamba hatua hiyo inaweza kuwahamisha wafanyikazi wengi kutorokea Uingereza. Hivi sasa kuna karibu Wakenya 900 wanaofanya kazi katika Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza katika nafasi mbali mbali , kulingana na mamlaka za Uingereza.
Nchi hizo mbili pia zimezindua Muungano wa Afya wa Kenya na Uingereza ambao utaongeza utafiti na ushirikiano kati ya Uingereza na vyuo vikuu vya Kenya na hospitali za mafunzo.Ushirikiano wa kwanza utasaidia kuboresha matibabu ya saratani nchini.