Wahudumu wa afya wa Kenya wasio na kazi wakubaliwa kufanya kazi nchini Uingereza

Hivi sasa kuna karibu Wakenya 900 wanaofanya kazi katika Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza katika nafasi mbali mbali , kulingana na mamlaka za Uingereza.

Muhtasari

•Waziri wa Afya wa Uingereza Sajid Javid na Waziri wa Kazi wa Kenya Simon Chelugui walitia saini makubaliano hayo hapo jana katika siku ya tatu ya ziara ya Rais Uhuru Kenyatta huko London.

•Lakini kuna hofu kwamba hatua hiyo inaweza kuwahamisha wafanyikazi wengi kutorokea Uingereza. Hivi sasa kuna karibu Wakenya 900 wanaofanya kazi katika Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza katika nafasi mbali mbali , kulingana na mamlaka za Uingereza.

Image: AFP

Kenya imesaini makubaliano na Uingereza ambayo yatawaruhusu wauguzi wake wasio na kazi na wahudumu wengine wa afya kufanya kazi nchini Uingereza.

Waziri wa Afya wa Uingereza Sajid Javid na Waziri wa Kazi wa Kenya Simon Chelugui walitia saini makubaliano hayo hapo jana katika siku ya tatu ya ziara ya Rais Uhuru Kenyatta huko London.

Mpango huo uko wazi kwa wafanyikazi wa afya wa Kenya ambao wamehitimu lakini hawana kazi, kuhakikisha mchakato huo unaifaidiKenya , kulingana na taarifa kutoka kwa serikali ya Uingereza.

Mpangilio huu uliombwa na Kenya na Unapaswa kuruhusu wataalamu na wasimamizi wa afya kufaidika na njia maalum kupitia mfumo wa uhamiaji wa Uingereza, kabla ya kurudi kazini katika sekta ya afya ya Kenya.

Maelezo kamili yanapaswa kuthibitishwa kabla ya mwisho wa Oktoba.Chama cha madaktari nchini Kenya katika miaka ya hivi karibuni kimeibua wasiwasi kuhusu kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kati ya madaktari na wauguzi nchini humo.

Makubaliano na Uingereza yanaweza kuwavutia wafanyikazi wengi wa huduma ya afya nchini Kenya kwani wamekuwa wakilalamikia hali mbaya ya kufanya kazi, malipo duni na hata kufanya kazi kwa miezi bila malipo.

Lakini kuna hofu kwamba hatua hiyo inaweza kuwahamisha wafanyikazi wengi kutorokea Uingereza. Hivi sasa kuna karibu Wakenya 900 wanaofanya kazi katika Huduma ya Kitaifa ya Afya ya Uingereza katika nafasi mbali mbali , kulingana na mamlaka za Uingereza.

Nchi hizo mbili pia zimezindua Muungano wa Afya wa Kenya na Uingereza ambao utaongeza utafiti na ushirikiano kati ya Uingereza na vyuo vikuu vya Kenya na hospitali za mafunzo.Ushirikiano wa kwanza utasaidia kuboresha matibabu ya saratani nchini.