Hizo ni picha halisi! Oparanya avuja kimya chake

"Hizo ni picha za ukweli kabisa. Sijui kwa nini mtu apoteze muda kujaribu kuzisambaza. Inasikitisha aliyepiga picha hizo na kuzisambaza kwa waandishi wa habari," alisema.

Muhtasari

• "Hizo ni picha za ukweli kabisa. Sijui kwa nini mtu apoteze muda kujaribu kuzisambaza. Inasikitisha aliyepiga picha hizo na kuzisambaza kwa waandishi wa habari," alisema.

Gavana Wycliffe Oparanya
Gavana Wycliffe Oparanya
Image: THE STAR

Aliyekuwa Gavana wa Kakamega amezungumzia picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na mwanamke Mary Biketi.

Katika video iliyowekwa kwenye mtandao Facebook, Oparanya alisema picha hizo ni za kweli, lakini alishangaa kwa nini mtu alichagua kuzisambaza.

"Hizo ni picha za ukweli kabisa. Sijui kwa nini mtu apoteze muda kujaribu kuzisambaza. Inasikitisha aliyepiga picha hizo na kuzisambaza kwa waandishi wa habari," alisema.

Aliongeza kuwa alikuwa akijitahidi kuelewa nia ya watu kuhusiana na picha hiyo, akisema ni nzuri.

Wakati huo huo, alikanusha madai kwamba alikuwa amelazwa hospitalini.

Oparanya alisema ana familia ambayo inahitaji ulinzi wake, akisema kuwa habari zozote za uwongo zinawaumiza.

"Nina familia kubwa ya kulinda hivyo wanaotuma habari za uwongo wakome. Hapa nilipo, nina uwezo wa kuongea, sina shida. Nimekuwa Mombasa kwa siku chache nikikutana na watu wangu wa jamii yangu," aliongeza.