Mke wa naibu gavana apatikana amefariki ndani ya nyumba

Masud ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Tanzania amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo kwa muda.

Muhtasari

•Mkewe Saisi, Ashura Masud Saisi alipatikana akiwa ameaga ndani ya nyumba na mmoja wa watoto wake.

Mkewe Patrick Saisi marehemu Ashura Masud
Mkewe Patrick Saisi marehemu Ashura Masud
Image: HISANI

Naibu gavana wa kaunti ya Vihiga Patrick Saisi alipoteza mkewe Alhamisi alasiri.

Mkewe Saisi, Ashura Masud Saisi alipatikana akiwa ameaga ndani ya nyumba na mtoto wake mmoja.

Masud ambaye ni mzaliwa wa nchi ya Tanzania amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya moyo kwa muda.

Msaidizi wa naibu gavana huyo alithibitisha taarifa hizo kwa simu.