In Summary

•Polisi upande wa Murang'a wanazuilia watu wanne waliopatikana wakisafirisha kilo 100 za pembe za ndovu zenye thamani ya shilingi milioni 10.

•Pembe hizo zilikuwa zimewekwa kwa gunia mbili na kufunikwa na mboga ikae kana kwamba ni mboga zilikuwa zinasafirishwa.

Washukiwa wa biashara haramu ya viungo vya wanyama pori
Image: TWITTER//DCI

Polisi upande wa Murang'a wanazuilia watu wanne waliopatikana wakisafirisha kilo 100 za pembe za ndovu zenye thamani ya shilingi milioni 10.

Wanne hao Martin Mungai (58), Peter Macharia (32), Edward Mwambura (55) na Samuel Njuguna (43) walikamatwa alasiri ya Jumapili baada ya kuhusishwa na biashara haramu ya viungo vya wanyamapori.

Kulingana na DCI wanne hao walikamatwa wakiwa kwa gari mbili tofauti wakiwa tayari kuendeleza biashara.

Pembe hizo zilikuwa zimewekwa kwa gunia mbili na kufunikwa na mboga ikae kana kwamba ni mboga zilikuwa zinasafirishwa.

Wanne hao wamezuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.

View Comments