In Summary
  • Hii ni baada ya mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, makamishna Abdi Guliye na Boya Molu kumtaka rais William Ruto kuunda tume ya uchunguzi
Mgombea wa useneta wa Nairobi Edwin Sifuna wakati wa kibali Kasarani.

Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna amewataka Wakenya wanaotoa madai ya machafuko ya Bomas kujiandaa kutoa ushahidi mbele ya tume ya uchunguzi ambayo bado haijaundwa.

Katika taarifa siku ya Jumanne, Sifuna alisema wanapaswa kuwa na uthibitisho wa madai hayo.

"Tuhuma nzito zinazotolewa kuhusiana na kile kilichotokea Bomas katika kuelekea kutangazwa kwa matokeo ya Urais," alisema.

"Ninatumai watu wanaowasilisha watafikishwa mbele ya tume ya uchunguzi ambayo bado haijaundwa na kutoa ushahidi unaounga mkono madai haya."

Hii ni baada ya mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, makamishna Abdi Guliye na Boya Molu kumtaka rais William Ruto kuunda tume ya uchunguzi.

Chebukati alisema uchunguzi huo utafichua fitina baada ya kura ya urais mnamo Agosti 9 katika Kituo cha Kitaifa cha Kuhesabu kura katika eneo la Bomas of Kenya.

"Matokeo ya Uchunguzi yataimarisha uhuru wa Tume na kuhakikisha kwamba inadumisha hadhi inayopendekezwa na Katiba ya Kenya," Chebukati alisema.

Hafla ya kustaafu rasmi kwa watatu hao kutoka IEBC iliandaliwa jijini Nairobi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo rais William Ruto ambaye awali amenukuliwa mara kadhaa akimtaja Chebukati kama shujaa aliyesimamamia ukweli katika uchaguzi wa Agosti mwaka jana.

Katika hotuba yake kwenye hafla hiyo, rais Ruto alisisitiza kuwa wana ufahamu kuwa kulikuwepo na njama na kumteka nyara mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati na kumuua baada ya kukataa kukubaliana na kile ambacho Ruti alisema ni kurubuni kwa matokeo ghushi ya kumtangaza mpinzani wake Raila Odinga kama rais.

“Pia tuna habari kuwa kulikuwepo na jaribio la moja kwa moja la kumteka nyara Wafula Chebukati na kumuua ili tume ya IEBC ilemazwe au kamishna mbadala achukue hatamu na kubatilisha kile ambacho wananchi walikuwa wameamua. Ulikuwa ni wakati mgumu, vitisho vilikuwa vingi, ahadi za kumezewa mate nyingi na shinikizo lilikuwa juu,” Rais Ruto alisema.

 

 

 

View Comments