In Summary

•Naserian alimwua kinyama binti yake wa miaka 2 kwa kumdunga kisu mara nyingi kisha kula sehemu zake za ndani.

Olivier Naserian aeleza sababu za kumuua bintiye
Image: Mpasho

Mwanamke mwenye umri wa miaka 24 ambaye alimuua na kula sehemu za mwili wa bintiye katika eneo la Kitengela ametaja matatizo ya kiakili kama kiini cha kitendo hicho. 

Amezuiliwa kwa siku kumi akisubiri uchunguzi zaidi kuhusu mauaji hayo ya kinyama ambayo yametamausha umma.

Mahakama mjini Kajiado siku ya Jumanne iliamuru kuzuiliwa kwa Olivia Naiserian ambaye anakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya kudaiwa kumuua bintiye wa miaka miwili.

Mwanamke huyo anasemekana kumkatakata mtoto wake vipande vipande kwa kisu kabla ya kula sehemu za viungo vyake vya ndani. Olivia Naserian anashtakiwa kwa mauaji ya bintiye Glory Njeri nyumbani kwao Kitengela mtaa wa Milimani siku ya Jumapili, Aprili 23.

Alianza kula sehemu za ndani za mwili wa bintiye  kabla ya majirani kuwaarifu polisi, ambao walifika eneo la tukio na kumkamata.  Kulingana na Gazeti la Nation mama huyo alitaja sababu za za kutekeleza mauaji hayo ya kinyama. 

Pia alilaumu mateso, bila kufafanua zaidi.

"Ninajichukia mwenyewe. Sijipendi ndio maana niliua mtoto wangu. Nimepitia magumu na huyu mtoto.," Bi Naserian alinukuliwa katika mahojiano na Nation.

Bila kuleza kwa kina mateso ambayo amepitia na mtoto wake, anaeleza kwamba alitaka kujitoa uhai lakini akabadili mawazo  na kumgeuzia bintiye kisu, akimchoma kisu mara nyingi, katika hali ya kutisha.

Kitendo cha kuhuzunisha cha mwanamke huyo kilirekodiwa na majirani waliojaribu kumwokoa mtoto huyo kwa kuvunja mlango lakini wakachelewa. Walipoingia, mtoto alikuwa tayari amekufa. Wazazi wake hawakuwa nyumbani wakati wa tukio hilo.

Kwa sasa Olivia anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kitengela huku wapelelezi wakiendelea na uchunguzi.

"Ni tukio la kushangaza. Tutakuwa tukimhoji ili kufahamu kiini cha mauaji hayo. Pia tunataka kujua ikiwa mauaji hayo yalikusudiwa," polisi walisema.

Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Jane Kamau Jumanne ambaye aliamuru abaki rumande kwa siku 10 ili kuruhusu maafisa wa polisi kukamilisha uchunguzi wao.

 

View Comments